Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha,
kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi
au kwa urefu. Angalia Msaada wa kuanzisha makala ili ujifunze
unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa
sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo
itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia,
ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili
kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Wolfgang Amadeus Mozart alikuwa mtunzi mashuhuri wa opera na mpigaji
wa ajabu sana wa piano kutoka nchini Austria alipolizaliwa katika jiji
la Salzburg tarehe 27 Januari 1756. Enzi za maisha yake mafupi,
aliandika zaidi ya tungo 600 za muziki. Watu wanaamini kwamba huyu ni
moja kati ya watunzi bora wa muda wote. Alitunga nyimbo kadhaa
zikiwemo opera (muziki wenye hadithi) Don Giovanni na Die Zauberflöte
(Filimbi ya Ajabu).
Kazi zake alizianza na minuet (dansi) aliyoitunga akiwa na umri wa
miaka minne, na alizimalizia kwa kipande chake cha mwisho, Requiem,
ambacho alikiacha hajakimaliza.
Mozart alikuja kufariki tarehe 5 Desemba 1791, akiwa na umri wa miaka 35.
Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!
Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya
maandishi huru.
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina
nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Asili yake ni aina
za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi
nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika
mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga
nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Maandishi yanapatikana chini ya leseni ya Creative Commons
Attribution/Share-Alike License; matakwa mengine yanaweza
kutakiwa. Tazama maelezo zaidi ya Matakwa ya Utumiaji.
